Jumatano , 22nd Jul , 2015

Wakati zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura likiwa limeanza rasmi hii leo Jiji la Dar es Salaam, mtayarishaji muziki mahiri Nahreel ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi.

msanii wa kundi la muziki la Navy Kenzo la Tanzania Nahreel

Mchango wa msanii na mtayarishaji muziki huyo, umeenda sambamba na maoni ya msanii Nikki Wa Pili ambaye amewataka vijana licha ya kushiriki kujiandikisha, kufuatilia sera za wagombea na mchakato mzima wa kampeni kwa makini ili kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa mustakabali wa taifa.

Hakikisha kijana mwenye umri wa kuanzia miaka 18 mwenye sifa na vigezo vyote kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam, haupitwi na nafasi hii ya kujiandikisha.
Zamu Yako 2015, Usichukulie poa, Kajiandikishe.