Vita ya Meek Mill na Nick Minaj yafikia pabaya

Alhamisi , 6th Feb , 2020

Kama umekuwa mfuatialiaji mzuri wa mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter, utagundua kuwa kuna bifu kati ya wapenzi wa zamani ambao ni Meek Mill na Nick Minaj.

Pichani ni Meek Mill na Nick Minaj enzi za mahusiano yao

Wawili hao wameiteka mitandao ya kijamii baada ya kurushiana maneno, ambapo Nick Minaj alianza kupost picha za zamani za Meek Mill kwenye insta story, huku akimshtumu kumuogopa kwa sababu ya kupiga wanawake.

"Umempiga Dada yako hadi ukafungwa, ukanipiga na mimi mbele ya Mama yako mzazi kisha ukatupeleka hospitali, unapiga hadi wanawake nakuogopa wewe mwanaume, umekuwa unamfuatilia mwanaume wangu kwa mwaka sasa kwenye mitandao ila amekublock, najua unaona aibu" ameandika Nick Minaj.

Baada ya post hiyo muda mfupi baadaye Meek Mill alimjibu kupitia mtandao wa Twitter ambapo ameandika  "Kwa ufafanuzi zaidi sijawahi kumpiga mwanamke, njia pekee ambayo utaweza kuiua kazi yangu ukisema napiga wanawake, mzungumziye Kaka yako ambaye amefungwa kwa makosa ya kubaka na amembaka mtoto mdogo kabisa, na kila mtu anakujua sasa kwamba wewe ni mtu mbaya".

Wawili hao waliwahi kuwa kwenye mahusiano kwa miaka miwili kuanzia 2015 hadi 2017, na habari zao za kutukanana mitandaoni zimeripotiwa na vyombo vikubwa vya habari nchini Marekani na duniani kwa ujumla.