Alhamisi , 9th Jul , 2015

Baada ya kutamba na kibao kikali katika video ya wimbo wao 'on My Way' wa msanii Jimwat akishirikiana na Das Walanguzi, wasanii hao wameungana na jeshi la wasanii Ala C na Jua Cali katika wimbo mpya uliobatizwa jina ‘Sema Nami’.

wasanii wa miondoko ya Genge nchini Kenya Ala C, Jimwat, Das Walanguzi na Jua Kali

Mastaa hao wa nchini Kenya wametoa kibao hicho kipya ambacho tayari kimekuwa gumzo katika vituo vya radio Afrika Mashariki huku mipango ya kuandaa kichupa ikiwa mbioni kufanyika.