Jumatatu , 29th Nov , 2021

Roma Mkatoliki ameweka wazi kwamba wasanii wa bongo wana ugomvi, chuki, husda bifu na visasi.

Picha ya msanii Roma Mkatoliki

Roma Mkatoliki ameshea hilo kwenye page yake ya Instagram na Twitter akishangaa mtu kufananisha bifu za wasanii wa Bongo kufikia bifu la waliokuwa wasanii wa HipHop nchini Marekani Tupac na Big Notorius.

"Ninapoona mtu anafananisha bifu za wasanii wetu wa home kwamba ipo siku itafika level ya bifu Ya Pac & Biggie huwa ninamshangaa sana"

"Ni kweli kuna wasanii wa home wana ugomvi,chuki,husda,visasi,bifu lakini haitaweza kufika level ya kina Pac, Bongo kuna ka-love bado kapo"