Jumatano , 31st Aug , 2016

Majaji wa Shindano la Dance100% linaloendeshwa na East Africa Television wanaendelea na shughuli ya kuwafundisha mbinu za kushiriki mashindano katika maeneo ya kambi zao wanazofanyia mazoezi.

Majaji katika shindano la Dance100%

Akizungumza na EATV mratibu wa shindano hilo Bhoke Egina amesema majaji hao wamegawana makundi hayo ambapo majaji huwafuata katika maeneo yao ya mazoezi ili kuweza kuzungumza nao na kuona namna wanavyofanya mazoezi na kuwafundisha na kuwashauri cha kufanya.

“Makundi yote kumi yana ratiba yao na majaji kulingana na namna walivyopangiwa mtu wa kuwafundisha, na zoezi hilo linaendelea vizuri , na mambo wanayofundishwa tutarajie kuyaona Septemba 03 watakapochuana katika nafasi ya nusu fainali” mmesema Bhoke.

Makundi hayo yanasimamiwa na majaji kama ifuatavyo. Jaji Super Nyamwela anasimamia makundi manne , BKK Boys, Tatanisha Crew, D.D.I Crew, na The Heroes Crew.

Jaji Lotus anafundisha makundi matatu: The Quest Crew, Mazabe Powder na Wazawa Crew.

Jaji Khalila anasimamia makundi matatu. Team Makorokocho, J Combat Crew, na Clevers Boys

Matukio yote ya Dance100% na namna makundi yanavyopambania ushindi wa shindano hilo yanaoneshwa na EATV siku ya Jumapili saa moja jioni chini ya udhamini wa Vodacom na Coca- Cola.

Kundi la Tatanisha Crew
Tags: