
Msanii kutoka lebo ya Wasafi RayMond Tiptop
Akikanusha fununu hizo Ricardo alisema kuwa si kweli kwakuwa kila msanii katika lebo yao huwa anajitungia nyimbo yeye mwenyewe "labda kusaidiana tu kimawazo".
“Hakuna anayemuandikia mwingine ila wanasaidizana wote kwa pamoja kila mtu ana uwezo wake na kila mtu anajiamini kwa kile anachokifanya”, alisema Ricardo.
Fununu zilizopo mitaani ni kuwa msanii Raymond ndiye muandishi wa nyimbo nyingi zadi katika lebo hiyo mpaka ngoma ya Bado iliyoimbwa na Harmonize ambayo alipokonywa na kupewa Harmonize.
Ricardo aliongeza kuwa awali wasanii hao wote nyimbo zao zilikuwa na jina moja la 'Bado' na wao wakaona haifai ndiyo wakaamua kutofautisha majina na kuita 'kwetu' na 'Bado'.
