Wolper amwandalia zawadi hii mpenzi wake

Jumanne , 8th Oct , 2019

Muigizaji na Mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper, amefunguka kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi ambayo ameamua kuyaficha bila kumuonyesha Mwanaume aliyekuwa naye kwa sasa huku akiwaacha watu midomo wazi.

Jacqueline Wolper

Alivyodakwa na camera za  EATV & EA Radio Digital, Wolper ameeleza kuwa yupo kwenye mahusiano ila hataki kuonyesha kwa sababu ya ubize wa kazi aliyokuwa nao na hawezi kuwa single.

"Mimi kwa kweli nilishajaribugi sana kuwa single lakini siwezi, sina sababu ya kuwa single nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini nipo bize sana na kazi kwa hiyo hata niliyekuwa naye anajua kama nazingatia sana kazi kuliko mapenzi na tunaelewana ila kuhusu kumpost nitampost siku ya Birthday yake", ameeleza.

Aidha akizungumzia zawadi ambayo amemuandalia Mwanaume wake kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake 'birthday' Jacqueline Wolper amesema,

"Zawadi yangu niliyomuandalia ni uwepo wangu kwake kwa sababu ana bahati ya kuwa na mimi ambaye ni Mwanamke haswa pia zawadi ambayo atayahitaji zaidi kutoka kwangu ni mapenzi ya dhati hivyo vitu vingine vitakuja tu" ameongeza.