Young Dee kama Young Thug

Alhamisi , 13th Mei , 2021

Rapper Young Dee yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha album yake mpya ijayo, na habari njema ni kwamba kwenye ujio huo utamsikia Dolly White ambaye ni Dada wa Rapper wa Atlanta, Georgia Young Thug.

Msanii Young Dee

Paka Rapper amethibitisha kupokea sauti (Audio Files) za collabo hiyo kupitia instagram kwa ku-post sehemu ya kipande cha video akisikiliza na kuambatanisha ujumbe wa kumpongeza Dolly kwa alichokifanya.

Young Dee amefanya kama Young Thug kwa Dolly ambaye yupo chini ya “Young Stoner Life” kwani aliwahi  kumshirikisha kwenye baadhi ya kazi pamoja na Lil Duke.