Sikutegemea kuwa na Baraka - Najma

Ijumaa , 14th Jul , 2017

Msanii wa muziki wa bongo fleva Najma ambaye ni mchumba wa Baraka The Prince amefunguka na kusema hakutegemea kuwa katika mahusiano na Baraka The Prince lakini alijikuta tu ameingia kwenye mahusiano na msanii huyo. 

Msanii Baraka The Prince akiwa na mpenzi wake Najma

Najma alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema awali hakutegemea kama angekuwa katika mahusiano na msanii huyo.

"Kiukweli kabisa mimi wala sikutegemea kuwa na Baraka The Prince sema imetokea, nashukuru Mungu tunapendana saizi yeye ndiye ananichagulia hata nguo za kuvaa akiona sijapendeza ananiambia hata kama kitu mimi nimependa yeye asipopenda nabadili, kwa hiyo tunapenda sana" alisema Najma 

Kwa upande wake Baraka The Prince alisema kuwa ni mapenzi ni moyo wa mtu wala si kabila au ushamba ni vile watu wawili mnavyopenda na kukubaliana na ndiyo kitu kilichotokea kati yao.

"Unajua mimi ni Msukuma na natoka Mwanza lakini nikwambie kitu mapenzi siyo kabila wala sehemu unayotoka, maana unaweza kuwa unatoka mkoani lakini ukawa mjanja na wapo wengine wanatoka mjini lakini washamba, kwa hiyo mimi na Naj tunapendana na tumekubaliana na ndiyo maana unaona tuko pamoja mpaka sasa" alisema Baraka The Prince.