Bibi wa miaka 90 alivyoishi bila mume

Jumatano , 25th Sep , 2019

Bibi mwenye umri wa 90 nchini Marekani aitwaye Claire, ameeleza sababu za kuishi miaka hiyo bila kuwa na Mwanaume.

Bibi huyo amefunguka hayo katika kipindi cha 'Love What Matters', ambapo amesema kuwa hali ya yeye kuishi kwa muda wote huo bila ya kuwa na mwanaume, imepelekea afya yake kuwa imara na kutokumbwa na magonjwa.

Licha ya kuwa ni maajabu kufikisha umri huu lakini bado nina furaha na afya napenda kuishi umri mrefu na sina magonjwa ya uzee,pia sina mawazo ya kuwa na mwanaume ambayo mara nyingi hufanya watu wasifikie umri huu" amesema Claire.

Claire ameongeza kuwa ameshashuhudia watu wengi wanawahi kupoteza maisha yao, kwa sababu ya kuendekeza mawazo kutoka kwa wapenzi wao kama vile usaliti.

Bibi Claire pia ameeleza siri iliyomfanya akae kando na wanaume ni pamoja na kutowapa nafasi ya kumuumiza na kuweka mipaka ya urafiki na jinsia hiyo, na kuamua kuishi maisha ya kwake pekee.

By Love What Matters