Ijumaa , 6th Sep , 2019

Kwa kawaida kila binadamu huwa na vidole vitano viganjani mwake na kidole gumba ndiyo kinakuwaga kifupi zaidi miongoni mwa vidole vyote.

Jacob Pina akionesha kidole gumba chake.

Hali imekuwa tofauti kwa Jacob Pina, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Westport nchini Marekani. Anatajwa kuwa na kidole gumba kirefu zaidi duniani.

Kijana huyo alionyesha kidole chake hicho kwa kutumia video fupi ambayo alipost katika mitandao ya kijamii na maelezo yake ni, "Hiki ni kidole gumba changu kiukweli ni kirefu sana siwezi kushindwa kama tukishindanishwa watu wenye vidole vikubwa na virefu, ili mukifikie kidole changu itabidi muonganishe vidole vya watu wa tatu"

Baadhi ya watu wali-comment kwa kuandika kidole hicho kitakuwa kimeeditiwa na 'filter', mwingine ameandika haamini anahitaji kuona mkono mzima.

Baada ya muda mfupi video hiyo ilienea zaidi mitandaoni na ilipata 'Likes' Milioni 2.1 na 'Comments' 37,400 pia aliongeza wafuasi katika mtandao wa kijamii wa Tik Tok ambako anatumia jina la @jwpina kutoka 'Followers' 75 hadi kufikia idadi ya 155,000.