Darassa ataja kisa chake na Baba yake

Ijumaa , 15th Mei , 2020

Kupitia kipindi cha SalamaNa kinachoruka East Africa TV, kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku, msanii Darassa amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yake, familia,shule, muziki, life style pamoja na changamoto zote.

Msanii Darassa

Kuhusu maisha ya familia yake Darassa amesema  "Baba yangu amekuwa na maisha yake kwa uzuri tu si kwa ubaya, tangu nimekuwa ni mimi na mama yangu, jambo hilo limenijenga kuwa mwanajeshi na hata kwenye maisha yangu sina chakumlaumu baba maana yeye ame-play part yake, najua ananihitaji na naishi naye kama mwanaume mwenzangu japo sio marafiki".

Aidha kwenye changamoto za kutoka kimuziki amesema, ameshakutana na Dully Sykes, na msanii wa kwanza kuwa na namba yake kwenye simu alikuwa ni Mwana Fa.

"Ilala kulikuwa na Dully Sykes kipindi hicho natoka Kiwalani, alikuwa anakusanya watu wanaojua kuimba pale Misifas Camp, kuna siku aliniuliza mbona hajawahi kunisikia nikiongea na ameniona kwa muda mrefu, Pia nilikuwa naenda hadi East Coast kwa ajili ya kumfuata Mwana Fa tu, ndiyo mtu wa kwanza kuwa na namba yake kama msanii kwenye simu yangu".