Fahamu faida za kutoa machozi kwenye maisha

Alhamisi , 1st Apr , 2021

Kupitia kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio Mwanasaikolojia George Boniphace amesema kutoa hisia zako kwa njia ya kutoa machozi kuna faida kubwa kwenye mwili wa binaadam.

Picha ya Mwanasaikolojia George Boniphace

"Watu tunatakiwa tujifunze kutoa hisia zetu kama kusikia huzuni, wivu, chuki au upendo tafuta njia ya kuvitoa, takwimu zinasema sababu zinazofanya wanawake kuishi sana ni kutokaa na vitu ambavyo wasipovizungumza basi watalia kwa hisia

"Kulia kule kwa hisia mtu anakuwa anatoa hasira vinyongo hivyo inamsaidia kujenga mwili wake kuwa mpya na kupata experince nyingine kwa wanaume hali hiyo haitukuti sana kwa sababu kuna jamii zingine zinaamini mwanaume akilia ni udhaifu" ameongeza Mwanasaikolojia George Boniphace.