Familia ya Bilionea Laizer yafafanua Bilioni 7.8

Alhamisi , 2nd Jul , 2020

Familia ya Bilionea mpya wa nchi Saniniu Laizer imesema familia yao imekuwa kwa nidham ya juu na ushirikiano mkubwa hivyo hawaoni sababu ya kuanzisha migogoro kwenye familia kisa pesa zake.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital kuhusu mgawanyo wa pesa hizo ndugu, mwanafamilia na meneja wa Bilionea Laizer aitwaye Kiria Laizer ameeleza kuwa 

"Kuhusu migogoro ya pesa inategemea familia yenu imekuaje, sisi familia yetu tumekua kwa nidhamu ya juu na kila kitu kipo kwenye ushirikiano, hakuna namna ambavyo pesa zake inaweza kuleta shida kwa familia, yeye amekua mtu wa ushirikiano mkubwa pia sisi tunakuwa na vikao kwa jambo lolote ili kuzungumza ikupata muafaka mzuri na hakuna mvutano wa familia kuhusu mali za Laizer"

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.