Jumanne , 26th Mar , 2019

Ushawahi kujiuliza kwanini mtu anakuwa na macho ya rangi tofauti mfano Blue, kijani, kijivu au brown!, au mtu ambaye si chotara akawa na nywele za kizungu, yaani zile zinazoitwa 'blonde'? Nakufahamisha juu ya watu hao wanaoitwa Melanesians

Ni nadra sana kukutana na mtu ambaye hana asili ya Uingereza akawa na nywele za 'blonde', hususan akiwa na rangi nyeusi ya ngozi. Lakini pia ni nadra sana na huenda ukashtuka ukikutana na mtu mwenye macho ya rangi tofauti na iliyozoeleka na wengi.

Melanesians barani Australia

Hii ni kawaida kwa watu wa jamii ya bara la Australia, watu hao wamekuwa na kitu ambacho mpaka sasa wanasayansi wamewaweka kwenye kundi la kipee, kutokana na utofauti wao na binadamu wengine.

Watu hao ambao hupatikana  katika visiwa vya Solomon, Pijin, Bislama, Papua, Indonesia Mashariki, Vanuatu na Fiji, wana upekee huo wa kuwa na macho ya blue na nywele za aina hiyo ya'blonde'.

Mtoto mwenye asili ya Melanesians

Watu hawa wanajulikana kwa jina la 'Melanesians', na mpaka sasa wanasayansi wameshindwa kujua kwa nini wana macho ya kipekee na nywele za utofauti na watu wengine wenye rangi nyeusi.

Hata hivyo vinasaba vya watu hawa haviko Australia pekee, kwani hata mabara mengine wapo ingawa ni kwa uchache sana, na iwapo utakutana nao lazima utapigwa na butwaa au ukadhani ni walemavu.

Miongoni mwa watu maarufu wenye upekee wa namna hii ni pamoja na msanii wa hip hop wa Marekani, Eminem, Muigizji Paul Walker, mcheza mpira wa Kikapu Steve Curry.

Msichana mwenye asili ya Melanesians