Jumatatu , 20th Dec , 2021

Mwanasaikolojia Cosmas Madulu, amesema kwamba mwanadamu anapobeba mambo mengi yanayozidi uwezo wake hupelekea kuchanganyikiwa ama kuugua magonjwa yasiyotibika.

Mwanasaikolojia Cosmas Madulu

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 20, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na kushauri kwamba ili kuepusha matatizo hayo, ni vyema watu kutoingia mwaka mpya na mambo ya zamani ambayo hayana tija kiroho na kimwili.

"Unatakiwa uanze mwaka kwa kuondoa mambo yote ya zamani, ambayo sio ya lazima kwenye roho na nafsi yako ili upate nafasi ya kuweka mambo mengine, hata simu inapojaa huwa haifanyi kazi vizuri," amesema Madulu