Jumanne , 21st Mei , 2019

Suala la kutunza pesa inaonekana kuwa ni changamoto kubwa sana kwa watu wengi, hii ni kutokana na kushindwa kujizuia na matumizi ambayo kwa kawaida yapo kila siku.

Kibubu

Japo katika jamii zetu kumekuwepo na baadhi ya makabila ambayo yanasifika kwa kutunza pesa zao wanazozipata, kwa namna nyingine huitwa 'wabahili'. Lakini ukweli ni kwanba mtu yoyote anaweza kutunza pesa zake akiamua kutokana na malengo aliyejiwekea.

Katika kipindi cha DADAZ cha EATV, Dkt. Hilderd Brandi Shayo ambaye ni Mtafiti na Mshauri wa Biashara na Uchumi Mbobezi wa bara la Afrika na Ulaya ameelezea njia nzuri ya kufanikiwa kwa wale wanaoweza kubana matumizi 'wabahili'.

Dkt. Shayo amesema kuwa mtu akiwa bahili na akapanga malengo yake ya kuyafikia baada ya kipindi fulani basi anao uwezekano mkubwa wa kufanikiwa.

Aidha amezungumzia namna nzuri ya ku'balance' matatizo ya ya kifamilia na malengo ya mtu aliyojiwekea ili kuweza kufanikiwa, "namna nzuri ya kuwasaidia ndugu zako, usiwape samaki, bali wape mshipi na ndoano waende wakavue wenyewe, hapo utakuwa umewasaidia na mwisho wa siku utakaa utaanza kuhesabu kuwa nimewsaidia watu fulani na wenyewe wataweza kuwasaidia wengine".

Tazama hapa chini Dkt. Shayo akizungumzia zaidi suala hilo.