Jumamosi , 27th Nov , 2021

Kijana mmoja nchini Kenya aitwaye Benson Kirobi, anamtafuta Baba yake aitwaye Benson Obote, ambaye hajawahi kumuona tangu azaliwe na kusema kwamba baba yake huyo alikuwa mwanajeshi na alitumwa nchini Sierra Leone kufanya kazi na hakuwahi kurudi tena.

Benson Kirobi, anayemtafuta Baba yake

Kufuatia hali hiyo Kirobi, aliamua kushika bango na kutembea nalo kwenye Jiji la Nairobi, akimtafuta mzazi wake huyo, ambapo wakati akifanyiwa mhojiano na Tuko swahili, alisema kwamba kwamba ameamua kufanya hivyo kwa kuwa kila mmoja hutamani kuwa karibu na watu anaowapenda.

"Baadhi ya watu walikuwa wakinitupia jicho kali, ishara kwamba kamwe hawakukubaliana na hatua yangu, hata hivyo nilihisi kuna wale ambao walinitia moyo kimya kimya, kila mmoja wetu anatamani kuwa na wale anaowapenda, ninaamini kwa kukutana naye, nitaelewa vyema kwa nini niko jinsi nilivyo,” amesema Kirobi

Kirobi  amesema kwamba baba yake alipoondoka nchini, mama yake alikuwa mjamzito na huenda hakuwa anafahamu hali ya mke wake huyo na kwamba mama yake Kirobi alipomuulizia aliaambiwa kwamba askari wengi waliokuwa kwenye oparesheni hiyo waliuawa vitani.