Jumapili , 8th Mei , 2022

Badala ya kuumiza kichwa ni biashara gani ya kufanya ambayo itakulipa vizuri na kubadilisha maisha, tambua kwamba pia unaweza kugeuza mapenzi yako na jambo fulani kuwa biashara.

Robert Franks (kushoto) akiwa na Fredo ambaye ni mshirika wake kwenye biashara ya viatu.

Ndugu wawili David Franks na Robert Franks walikuwa wanapenda sana viatu, walifungua youtube channel kwa ajili ya kuelezea viatu na baadae wakaanza kuuza viatu mdogo mdogo mtandaoni. Mpaka sasa youtube channel yao imeshatazamwa mara million 21.

Mwaka 2019 walifungua duka lao la kwanza nchini Uingereza @kickgameuk na walitegemea sana mitandao ya kijamii kwa kutengeneza video zinazoelezea viatu na kupelekea kupata mashabiki wengi mtandaoni nchini Uingereza.

Mwaka 2020, David na Frank walipata dili ya nono ya udhamini wenye thamani ya pauni millioni 3.5 sawa na Tsh billioni 10 kutoka kampuni ya VGC Firm, na kufungua maduka matano ya viatu nchini Uingereza huku wakiwa wameajiri watu 25 katika kampuni yao. Wanatarajia kutengeneza zaidi ya pauni millioni 50 mwaka huu kutokana na mauzo ya viatu.