Ijumaa , 9th Jun , 2023

Kampuni mpya ya pedi ya Luna Pads wameshiriki kumthamini binti anayepata changamoto ya kujisitiri kipindi akiwa kwenye hedhi kwa kuchangia taulo za kike 50 ili kumbakisha binti shuleni.

Balozi wa kampeni ya Namthamini, Justine Kessy akipokea taulo za kike kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Luna Pads, Luna Kikuchi.

Mchango huo umewasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bi Luna Kikuchi kutokea kampuni hiyo inayopatikana Kibaha Kwa Mfipa Mkoa wa Pwani.

Kampeni ya Namthamini 2023 ilizinduliwa Mei 28 mwaka huu, ikiwa ni msimu wa 7 tangu ianzishwe.