Jumatano , 25th Aug , 2021

Baadhi ya madaktari wameonya wale wanaoshiriki wa “Milk Crate Challenge” kwa sababu ya usalama wa kiafya kuwa mdogo kutokana na urefu wa kuelekea juu wa kreti hizo.

Picha ya washiriki wa Milk Crate Challenge

Madaktari wanasema kuwa upo uwezekano mkubwa wa washiriki kupata madhara makubwa pindi ambapo lengo litashindwa kukamilika kwa usahihi ikiwa hata kuvunjika shingo au mgongo.

Challenge hiyo ya kupanda juu ya kreti imeibuka siku za hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii huku kukiwa na idadi kubwa zaidi inayoonyesha washiriki wakipata majeraha mabaya.