''Makanisa yawe gereji'' - Goodluck Gozbert

Ijumaa , 6th Sep , 2019

Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Goodluck Gozbert amesema kuwa, Nyumba za Ibada hazipaswi kuwa kama Ofisi za Serikali, badala yake ziwe kama Gereji ambazo zitakuwa tayari kumpokea mtu wa aina yoyote ile na kumbadilisha kuweza kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Goodluck Gozbert

Goodluck ameyabainisha hayo leo Septemba 06, 2019 katika kipindi cha DADAZ cha East Africa Television.

''Inabidi tujue utofauti kati ya ofisi za Serikali na Kanisa, Ofisi zote za kiserikali ukienda kuna namna ya uvaaji wao, namna ya muonekano,  unyoaji wao, usipozifuata hizo utatoka, isifike hatua kanisa likawa kama Serikali,  hapana iwe gereji ya mtu anakuja vile alivyo unamuambia karibu sana mfundishe neno la Mungu ataona hivi nilivyo mbona nazingua atabadilika na roho wa Mungu atamsaidia kubadilika'' amesema Goodluck.

Akizungumzia namna ambavyo uimbaji wake umeweza kubadili maisha ya vijana wengi,  Goodluck amesema kuwa hana kitu chochote kinachowafanya vijana wamrudie Mungu bali maisha yake ndiyo hamasa kwa watu wengine kubadilika na kumfuata Mungu.