Mama azaa mjukuu wake

Jumanne , 2nd Apr , 2019

Mama mmoja mkazi wa Marekani mwenye miaka 61 anayejulikana kwa jina la Cecile Reynek Eledge, amezaa mtoto ambaye ni mjukuu wake wa damu.

Bi Cecile akiwa na mtoto wake wa kiume na mume wake

Tukio hilo limewezakana baada ya mtoto wake wa kiume anayejulikana kwa jina la Matthew anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja (shoga) kutaka kupata mtoto na mwenzi wake, Elliot Dougherty, ambapo alimtaka mama yake awazalie mtoto huyo.

Mama akubali ombi la kumzalia mwanae

 

Baada ya mama huyo kukubali kuwa 'surogate mother' kwa mjukuu wake, dada wa Elliot ambaye ni mume wa mtoto wake, akatoa yai lake ili kuchavushwa mbegu za kiume za mwanaye Mathew, kisha kubeba mimba ya mjukuu wake mpaka pale alipozaliwa siku ya jana Aprili 1, 2019.

“Ukiwa shoga na unataka kuwa na mtoto, utatakiwa ufikiria namna ya kipekee ya kupata watoto wako, kuna njia za kipekee za kutengeneza familia yako, zaidi ya yote, tunajihisi wenye bahati kupata mtu wa kutufanyia hili”, alisikika baba wa mtoto huyo Matthew Eledge, huku pembeni akiwa na mwenzi wake Elliot Dougherty.

Mathew ambaye kitaaluma ni Mwalimu, amesema kwamba alipata watu wengi chuoni ambao walikubali kumzalia mtoto, lakini alikuwa na ugumu kidogo.

Eliot ambaye ndiye mume huku akiwa na taaluma ya kutengeneza nywele, amepost kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kwamba anafurahi wanawake hao kuwa sehemu muhimu kwenye maisha yake.

Mathew akiwa na mume wake na mtoto wake ambaye amemzaa mama yake mzazi