Mboni Masimba aolewa na Tajiri

Ijumaa , 6th Sep , 2019

Mrembo na mtangazaji wa muda mrefu nchini, Mboni Masimba amefunga ndoa leo na mpenzi wake Ally Tajiri, ambaye sasa amekuwa mume wake.

Mboni Masimba na mume wake Ally Tajiri

Ndoa hiyo imefungwa kwa siri leo Septemba 6, 2019, Masaki jijini Dar es salaam na kuhudhuria na marafiki wa karibu wa Mboni.

Mpenzi wake huyo anayefahamika kwa jina la Ally Tajiri, imeelezwa kuwa muda mwingi anaishi nchini Uingereza, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa Mboni kuhamia nchini humo kwaajili ya kuanza maisha ya ndoa na familia.