Mbunge akiri kuvuta bangi Bungeni

Alhamisi , 24th Jan , 2019

Gavana wa Jimbo la Nairobi nchini Kenya, Mike Sonko amekiri vitendo vya kuvuta bangi ndani ya Bunge akiwa na mbunge mwenzake, wakati akitumikia Ubunge jimbo la Makadara.

Mike Sonko

Mike Sonko amefunguka hayo kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari vya Kenya, na kusema kwamba  wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda mrefu na muda mwengine hata kutumia bangi moja kwa kupokezana.

Sonko ameendelea kusimulia kuwa walikuwa wakitoroka wakati vikao vikiendelea na kwenda chooni, kisha kuvuta bangi kwa siri na kisha kurudi ndani kuendelea na vikao vya Bunge.

“Tulipokuwa Wabunge mimi na (akimtaja mwenzake), tulikuwa tukivuta bangi chooni, yeye alikuwa akizificha kwenye soksi, mimi sasa hivi nimeacha, lakini yeye bado anavuta”, amesema Gavana huyo wa jimbo la Nairobi.

Alipoulizwa kama anao ushahidi wa hayo Sonko alikiri kuwa ana ushahidi kwani walikuwa wakivuta wote, na kuwa sio jambo geni kwake.