Alhamisi , 7th Oct , 2021

Abdulrazak Gurnah huwenda likawa ni jina jipya kabisa masikioni mwako ila huyu ni Mtanzania aliyezaliwa Zanzibar mwaka 1948 ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Kent, Uingereza na mtunzi maarufu wa vitabu ambaye amefanikiwa kushinda tuzo ya Nobel ya Fasihi 2021 huko Stockholm nchini Sweden.

Picha ya mwandishi wa vitabu Abdulrazak Gurnah

Tuzo hiyo inamfanya kuwa Mwafrika wa pili kushinda na imetangazwa mapema wiki hii na Mats Malm ambaye ni katibu wa kudumu wa Swedish Academy na katika uandishi wake unatajwa kuchochea mabadiliko makubwa kwenye Jamii ikiwemo kuelezea athari za ukoloni na hatima ya wakimbizi.

Gurnah ameandika riwaya takribani 10 kama 'Memory of Departure', ‘The Last Gift’, 'Paradise' na kadhalika huku Tuzo ikiambatana na medali ya dhahabu na fedha taslimu dola Milioni 1.14 ambazo ni zaidi ya Tshs. Bilioni 2.62.