Salama kuja na kipindi kipya EATV

Jumatatu , 20th Jan , 2020

Mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni nchini Tanzania, Salama Jabir anakuja na kipindi kipya cha TV hivi karibuni, kitakachojulikana kwa jina la 'SALAMANA'.

Salama Jabir

Kipindi hicho ambacho kinawalenga zaidi vijana wenye umri wa miaka 18-35, kitaruka East Africa Television (EATV).  Kitakuwa kinahusu mazungumzo mbalimbali na marafiki zake, watu maarufu wakiwemo wanamuziki, waimbaji, wachekeshaji, wafanyabiashara na wengineo.

Stori hizo zinalenga kuelimisha, kuchekesha na kuburudisha. Kipindi kitakuwa kinaruka kila Alhamis Saa 3:00 Usiku hadi 4:00 Usiku kupitia Ting'a namba moja kwa vijana EATV. Marudio yake yatakuwa yakiruka kila Ijumaa Saa 8:00  Mchana na Jumapili Saa 8:30 Mchana.

SALAMANA, itaruka kwa mara ya kwanza Januari 30, 2020 EATV Pekee.