Sheikh Kipozeo amsihi msanii huyu kuhusu wanawake

Jumatano , 22nd Jan , 2020

Hilal Shaweji maarufu kama Sheikh Kipozeo, amemshauri msanii wa HipHop Stamina juu ya kukimbiwa na mkewe na kumsihi atafute mwanamke mwingine kama amevunjiwa heshima ndani ya ndoa yake.

Picha ya Sheikh Kipozeo

 

Sheikh Kipozeo ameeleza hayo wakati akipiga stori na big chawa, kupitia show ya Planet Bongo ambayo inaruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 7:00 mchana hadi 10:00 jioni.

"Mimi namuhusia tu kwamba wanawake wapo wengi, kwahiyo ukiona mwanamke anakuvunjia heshima unatafuta mwingine tu, japokuwa yule aliyepita si kama wa huyu atakayempata sasa hivi, lakini utamzoea tu na atakuwa kama yule, sio jambo la kusikitika sana ndiyo maana Mungu amewaleta wanawake wengi duniani kuliko wanaume" amesema Sheikh Kipozeo.