Shilole ataka heshima kwenye kazi yake

Jumatatu , 7th Oct , 2019

Msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali wa chakula, Shilole amewataka watu kuanza kuheshimu biashara yake na jinsi alivyopambana kuisimamisha.

Shilole

Amesema hayo kufuatia posti yake katika mtandao wa Instagram ikionesha jinsi sehemu hiyo ilivyokuwa kabla na baada ya kuanzisha biashara ya chakula ambayo inampa mafanikio makubwa hivi sasa.

Akipiga stori na Big Chawa kutoka Planet Bongo ya EA Radio, Shilole amesema, "haikuwa rahisi hapa kupaweka hivi, palikuwa pori tu lakini watu wanaweza kuona tu Shishi ana sehemu ya kuuza chakula."

"Sio rahisi kuona tu mnakaa kama hivi mmetulia mnakula AC lakini nimepambana, ndiyo maana nimeweka picha ya kabla na baada, kwahiyo watu tuheshimiane".

Akizungumzia juu ya wasanii wa kike wenye pesa nchini, Shilole amesema kuwa inawezekana yeye yupo miongoni mwa 10 bora lakini wenye kupanga hivyo vigezo ndio wanajua yeye wanamuweka namba ngapi.