Simama na mimi yazinduliwa rasmi

Jumatatu , 13th Jul , 2020

Ile kampeni ya "Simama na Mimi' iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu takribani wiki mbili sasa hatimaye imezinduliwa leo katika studio za East Africa Radio na East Africa TV, Mikocheni, Dar es Salaam.

Rais wa Bongo Fleva, Dullah Planet akikabidhiwa funguo ya gari na Mkuu wa Idara ya Masoko wa East Africa Television Ltd, Roy Mbowe.

Kampeni hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwatambulisha vinara wa East Africa Radio katika nyanja mbalimbali kwa wasikilizaji na wafuatiliaji wetu popote walipo duniani.

Akizindua kampeni hiyo, msimamizi wa mkutano wa leo ambaye ni mtayarishaji wa kipindi cha Planet Bongo, Grayson Gideon amesema kampeni itakuwa na mabalozi wanne wa mwanzo ambaye ni Dullah Planet (Rais wa Bongo Fleva), Maryam Kitosi (Mwanamke Kinara), Samson Charles (Mchambuzi Mkuu Siasa) na Ibra Kasuga (Mtaalamu) katika masuala ya michezo.

Kwa nyakati tofauti tofauti, mabalozi hao wameishukuru East Africa Television L.t.d pamoja na East Africa Radio kwa kuanzisha kampeni hiyo na kuahidi kujitoa kwa moyo wote. 

Tazama tukio nzima la uzinduzi wa Simama na Mimi hapa chini.