Stamina afunguka kuhusu kumuomba msamaha mkewe

Jumatatu , 1st Jun , 2020

Mkali wa HipHop Bongo Stamina, amefunguka na kusema suala la kuombana msamaha na aliyekuwa mkewe  ni jambo la siri na watu wawili, kwani wakati wanakubaliana kuwa kwenye mahusiano hakuwaambia watu.

Msanii Stamina akiwa na mkewe

Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital Stamina amesema  "Mimi sijaweka mahusiano yangu wala kumuonyesha mke wangu, ule ni mziki tu halafu sijui kwanini Watanzania hawaamini kwamba naweza nikamuimbia mtu mwingine, nimeongelea ndoa sijamuongelea mwanamke wangu".

"Masuala ya kuombana msamaha ni mambo binafsi ya watu wawili, kama yeye ameomba msamaha au mimi nimeomba msamaha ni vitu binafsi na hata ikitokea hivyo lazima ianze kwa watu wawili siwezi kuja kuvisema hadharani kwa watu".

Mahojiano kamili tazama kwenye video hapa chini.