Jumamosi , 9th Dec , 2023

Kama ulikwisha wahi kusikia ''Nataka nitoke na mpenzi wangu Sea'', Basi tambua yule ni PAPII KOCHA & NGUZA ambao ni baba na mwana.

Pengine makazini kuna idadi kubwa ya watu ambao wanafanya kazi ambayo hawaipendi na hii ni kwa sababu ya msukumo wa wazazi,

Mtoto huwenda alikuwa anandoto zake lakini wazazi wanataka mtoto afate ndoto zao, hawa ni baadhi ya wachezaji ambao watoto wao pia walikuwa wachezaji mpira wa miguu.

Alf-Inge Haaland baba wa mchezaji wa Manchester city Erling Haaland ambao wote wameichezea timu ya Man city

Carlos Mac Allister baba wa mchezaji wa timu ya Liverpool Alexis Mac Allister ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa mpira wa miguu ambaye aliwahi kuichezea Boca Junoir akihudumu kama beki wa kushoto.

George Weah mwanasiasa na mchezaji wa zamani Chelsea na Man city ambaye ni Baba mzazi wa mchezaji Timothy Weah mchezaji wa Juventus

Unaweza pia ukaongezea na wengine, lakini msingi wa haya yote ni kukuuliza kuwa unatamani mwanao afanye kazi kama yako?