Jumanne , 27th Apr , 2021

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Cameroon Alex Song ameiwezesha timu Arta Solar kutwaa ubingwa wa Djibouti baada ya miaka 40.

Alex Song

Song ambaye uamuzi wake wa kujiunga na timu hiyo ulizua mjadala mkubwa duniani kutokana na wasifu wake mkubwa wa kuchezea vilabu vikubwa duniani kama Arsenal 2007-2012 na Barcelona 2012-2016 kwa mafanikio makubwa, pia timu ya taifa ya Cameroon 'The Indomitable Lion' 2005-2014.

Mchezaji huyo alijiunga akiwa huru baada ya kuvunja mkataba na timu ya FC Sion ya Uswiss kutokana na ukata mara baada ya janga la corona kuingia, alifanya maamuzi magumu ya kujiunga na timu ya daraja la kati na kwenye taifa ambalo halijafanikiwa sana kisoka.

Song ambaye ni mpwa wa nyota wa zamani na nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Rigorbet Song, alitabiriwa kufanya makubwa, hasa baada ya kujiunga Arsenal akiwa mdogo na baadaye kutimukia Barcelona alipokuwa na nyota kadhaa wakubwa akiwemo Lionel Messi.

Kurejea kucheza Africa na hasa kwenye taifa lisilofanikiwa kisoka ilikuwa kama kashfa flani kwake lakini juhudi zake yeye kama nahodha wa timu hiyo, na wenzake zikawapa ubingwa.

Ikumbukwe katika msimu wa 2020/21 timu hiyo waliwahi kutolewa katika kombe la shirikisho la soka Africa na Arab Contractor ya Misri kwa jumla ya magoli 10-1.