Alhamisi , 30th Dec , 2021

Kocha wa Arsenal, The Gunner, Mikel Arteta atakosa mchezo wa Jumapili dhidi ya Manchester City ambapo utakuwa mchezo wa kwanza wa mwaka kwa timu hizo mbili, baada ya kubainika na maambukizi ya UVIKO-19.

Kukosekana kwa Muhispania huyo, inatoa taswira kuwa makocha wasaidizi Albert Stuivenberg na Steve Round watakuwa wasimamizi wa mchezo huo wa January 1 utakao chezwa kwenye uwanja wa Emirates.

Mpaka sasa Arsenal wameshinda mitanange minne mfululizo na kufanikiwa kukaa nafasi ya nne kwenye msimamo wa EPL, wakiwa alama 12 myuma ya Maningwa watetezi Manchester City.

Mchezo wa Duru ya kwanza kati ya timu hizo mbili, ulimalizika kwa Arsenal kuadhibiwa kwa kipigo cha mabao 5-0.