Ijumaa , 20th Jul , 2018

Kamati ya mashindano ya Sprite Bball Kings kupitia kwa mratibu wa mashindano Yohana Komba, imesema kila kitu kipo sawa kuelekea mechi za robo fainali ya michuano hiyo kesho Julai 21.

Msanii Aslay

Komba amesema tofauti na mechi za hatua zilizopita, robo fainali itanogeshwa na mambo mbalimbali ikiwemo burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Bongofleva  ambao watakuwepo kuunga mkono timu wanazozishabikia. 

''Kesho mambo yatakuwa vizuri sana kwanza burudani ya kinywaji baridi cha Sprite ambao ndio wadhamini wetu lakini msanii Aslay pia atakuwepo na wengine bila kusahahu zawadi kwa mashabiki watakaohudhuria'', - amesema.

Kwa upande wao shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF),  kupitia kwa kamishna wa ufundi na mashindano Manase Zabron, ameeleza kuwa waamuzi wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanachezesha kwa usawa na haki ili anayestahili kwenda mbele aende.

Mechi za kesho zitaanza saa 6:00 mchana hadi saa 2:00 usiku kwenye uwanja wa ndani wa taifa. Dimba litafunguliwa na timu za Water Institute  Vs Flying Dribblers huku Team Kiza dhidi ya DMI kabla ya mabingwa watetezi Mchenga Bball Stars kuvaana na St. Joseph na Temeke Heroes Vs Portland.

Timu ya Portland

Washindi wanne wa kesho watatinga hatua ya nusu fainali kabla ya timu mbili kuingia fainali tayari kwa kuiwania zawadi nono ya bingwa ambayo ni milioni 10 na mshindi wa pili milioni 3 huku 'MVP' akichukua milioni 2. Njoo tuirudishe heshima ya kikapu Bongo.