
Pierre-Emerick Aubameyang amefunga mabao 11 kwenye michezo 17
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 10 ya mchezo huo, hili ni bao lake la 9 kwenye La Liga katika michezo 11 aliyocheza tangu alipojiunga na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari kwa ujumla kwenye michuano yote amefungwa mabao 11 katika michezo 17.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa Barcelona baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo iliyopita dhidi ya Eintrancht Frankfurt kwenye michuano ya Europa League na mchezo wa Ligi dhidi ya Cadiz.
Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa jana
FT: Levante 2-3 Sevilla
FT: Espayol 0-1 Rayol Valcano
FT: Cadiz 2-3 Athletics Bilbao
Muonekano wa msimamo wa La Liga timu 4 za juu na alama zao
1. Real Madrid 78
2. Fc Barcelona 63
3. Sevilla 63
4. Atletico Madrid 61