Alhamisi , 15th Dec , 2016

Kiungo machachari wa Simba Awadhi Juma ameachana rasmi na klabu hiyo na kujiunga rasmi na wachimba madini wa Mwadui, Mwadui FC ya Shinyanga baada ya kukosa namba kunako klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi.

Awadhi Juma akiwa Simba msimu uliopita

Uongozi wa Mwadui FC umethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa katika usajili wake wa dirisha dogo, timu hiyo imesajili jumla ya wachezaji wapya 5 wakiwemo wawili kutoka klabu ya Simba.

Katibu Mkuu wa Mwadui FC amesema kuwa klabu hiyo imefuata taratibu zote za usajili, na kukubaliana na uongozi wa Simba ambao umetoa baraka na nyaraka zote muhimu za usajili. 

Awadhi ambaye alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar, amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza tangu aingie Msimbazi ambapo tangu msimu huu uanze hajacheza mechi hata moja.