
Kocha wa Azam FC Zeben Hernandez akimkabidhi Jezi Beki wa kati wa Klabu hiyo Yakubu Mohammed aliyetokea nchini Ghana.
Akizungumza wakati wa kuwatambulisha wachezaji hao, Afisa Habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema, wameshamalizana na wachezaji hao ambao ni beki wa kati Yakubu Mohammed akitokea Aduana Stars ya nchini Ghana, kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo aliyetokea Coton Sports ya Cameroon na winga Joseph Mahundi aliyekuwa akichezea klabu ya Mbeya City.
Jaffary amesema, Mohammed ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu amesajiliwa ili kuziba nafasi ya Pascal Wawa, huku Mpondo kwa upande wake akisaini mwaka mmoja na kwa upande wa winga wakiamua kumrejesha Mahundi aliyekulia Azam Academy ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Mbeya City alipomaliza mkataba.
Kocha wa Azam FC Zeben Hernandez akimkabidhi Jezi Kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo aliyetokea Coton Sports ya Cameroon
Maganga amesema, wanaamini ujio wa nyota hayo utazidi kuipa nguvu timu ya Azam FC kuelekea mzunguko wa pili wa igi kuu unaotarajia kuanza mwishoni mwa wiki hii, Kombe la Shirikisho (FA), na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederations Cup) hapo mwakani.
Wakati huo huo, Maganga amesema wameshafikia makubaliano ya kuachana na kiungo mkabaji raia wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’, ambaye amepata timu nchini Vietnam na muda wowote kuanzia sasa atakwenda huko.
Kocha wa Azam FC Zeben Hernandez akimkabidhi jezi winga Joseph Mahundi aliyekuwa akichezea klabu ya Mbeya City