'Baada ya wiki tutaangalia kuruhusu michezo' - JPM

Jumapili , 17th Mei , 2020

Rais Magufuli amesema kuanzia wiki ijayo kama maambukizi ya Corona yataendelea kupungua, atafikiria kufungua Vyuo na kuruhusu michezo iendelee.

Rais Magufuli

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akitoa salamu baada ya kushiriki kwenye Kanisa la KKKT Chato, mkoani Geita, ambapo atafikia uamuzi wa kurejesha michezo kwa kuwa michezo ni burudani kwa Watanzania.

Rais Magufuli amesema kuwa "kwa trendi hii ninavyoiona kama wiki hii inayoabnza kesho hali itaendelea kupungua nimepanga kufungua Vyuo ili wanafunzi waendelee kusoma, lakini pia tumepanga kuruhusu michezo iendelee."

Tazama video kamili hapo chini