
Luis Suarez
Suarez aliifungia Barcelona bao katika mchezo huo dhidi ya Athletic Bilbao ambao ulishuhudia wachezaji watatu wakipewa kadi nyekundu na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 iliyofanya Barcelona kufuzu fainali ya nne mfululizo kwa jumla ya mabao 3-2.
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alitolewa nje kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu aliyokaa Barcelona baada ya mwamuzi kudhani kuwa alimpiga kiwiko Koke katika dakika za majeruhi.
Suarez amesema kadi hiyo aliyopewa inamfanya ajisikie kucheka kwani inaonekana kama mwamuzi alidhamiria kufanya hivyo, na kusema kuwa wanataka kuona kama wanaweza kukata rufaa kwasababu hadhani kama alifanya kosa lolote kustahili adhabu hiyo.