
Eric Garcia
Garcia mwenye umri wa miaka 20, anajiunga na wababe hao wa katalunya akiwa mchezaji huru ambapo mkataba wake na Manchester City unamalizaika mwisho mwa mwezi Juni na atasaini mkataba na Barcelona utakao anza Julai 1, 2021 na utamaliza mwishoni mwa msimu wa 2025-26. Na katika mkataba wake kimewekwa kipenge cha ada ya uhamisho ya Euro milioni 400 kwa timu itakayootaka kuvunja mkataba wa mchezaji huyo ambayo ni zaidi ya Trilioni moja kwa pesa za kitanzania.
Beki huyo raia wa Hispania kabla ya kujiunga na Manchester City mwaka 2017 alikuwa seheumu ya timu ya vijana ya FC Barcelona La Masia na alikuwa mchezaji wa timu hiyo toka mwaka 2008, hivyo anarejea tena baada ya misimu minne japokuwa sasa anarejea na amesajiliwa kama mchezaji wa kikosi cha kwanza.
Disemba 18, 2018 alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City kwenye michuano ya kombe la Ligi (EFL Cup) hatua ya robo fainali dhidi ya Leicester City, lakini mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England EPL alicheza Septemba 21, 2019 dhidi ya Wataford. Mpaka anaondoka Manchester City kacheza jumla ya michezo 35 huku akiwa ameshinda jumla ya mataji matatu ikiwemo ubingwa wa EPL msimu uliomalizika wa 2020-21.