
Bayern Munich wakiwa wanashangilia ubingwa baada ya kubeba kombe la DFL Super Cup 2021 kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dormund usiku wa jana.
Bayern ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 41 lililofungwa na mshambuliaji wake Robert Lewandowski huku Thomas Muller akafunga bao la pili dakika 49 kabla ya Marco Reus wa Dortmund kufunga bao dakika 64 na dakika ya 74 Lewandowski akafunga bao la tatu kwa Bayern.
Ubingwa huo ni wa kwanza kwa kocha mpya wa Bayern, Julen Nagelsman aliyejiunga rasmi na Bayern mapema mwezi uliopita na kuwafanya Bayern kushinda kombe la saba la fainali hizo na kuendelea kuwa mabingwa wa kihistoria ilhali Dortmund wameshinda kombe hilo mara tatu.