Jumatatu , 9th Jul , 2018

Msanii wa Bongofleva Beka Flavour, amefurahia mashindano ya mpira wa Kikapu Sprite Bball Kings, yanayoandaliwa na East Africa Television LTD na kudhaminiwa na kinywaji cha Sprite, baada ya kuhudhuria mechi za hatua ya 16 bora zilizofanyika Julai 8 kwenye uwanja wa Bandari Kurasini.

Msanii Beka Flavour

Beka ameeleza kuwa mashindano hayo yameuamsha mchezo wa Kikapu ambao ulikuwa umeanza kushuka thamani pamoja na vijana wengi kutoupa kipaumbele licha ya kuwa ni moja ya mchezo unaotajirisha watu katika nchi Ulaya na Marekani.

''Mchezo wa soka ndio umekua ukipewa nafasi sana hapa nchini lakini East Africa Television mmefanya kitu cha tofauti kwa kuwakumbuka vijana wenye umri kuanzia miaka 16 kwa kuwaboreshea mchezo huu ambao kwa nchi za nje umetajirisha watu wengi'' - amesema.

Beka ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na kuwekeza kwenye mchezo huu kama ambaVyo kampuni ya Cocacola kupitia kinywaji baridi cha Sprite ilivyoungana na East Africa Televison LTD katika kurudisha heshima ya mpira wa Kikapu nchini.

Mashindano hayo kwasasa yamefikia hatua ya robo fainali baada ya mechi za 16 bora kukamilika jana jumapili Julai 8 kwenye uwanja Bandari Kurasini. Timu ambazo zimefuzu hatua hiyo ni St. Joseph, DMI, Portland, Water Institute, Mchenga Bball Stars, Temeke Heroes, Flying Dribblers na Team Kiza.

Droo ya kupanga mechi za hatua ya robo fainali inafanyika leo na itaruka moja kwa moja kupitia kipindi cha 5Sports cha East Africa Television na The Cruise ya East Africa Radio kuanzia saa 3:30 usiku.