Kocha mpya wa Everton Raphael Benitez
Benitez anachukua nafasi iliyoachwa na kocha Carlo Ancelotti aliyeachana na Everton na kutimkia katika klabu ya Real Madrid ya Hispania. Takribani wiki 3 zilizopita mashabiki wa Everton walionyesha nia yakutomtaka kocha huyo raia wa Hispania kuwa kocha mpya wa klbau hiyo kwa sababu aliwahi kuwa kocha wa maasimu wao klabu ya Liverpool.
Kocha huyo Mwenye umri wa miaka 61 alifanya kazi katika kikosi cha Liverpool kwa miaka sita (6) kati ya mwaka 2004 hadi 2010 ambapo alishinda jumla ya mataji manne ukiwemo ubingwa wa klabu bingwa ulaya msimu wa 2004-05.
Na Benitezi anakuwa kocha wa pili kwenye historia kuvifundisha vilabu vya Liverpool na Everton, ambapo kocha wa kwanza kufanya hivyo alikuwa William Edward Barclay, ambyaye aliifundisha Everton mwaka 1888 na baadaye Liverpool mwaka 1892.







