
Wachezaji wa timumbalimbali kutoka EPL wakionekana na jezi zao mpya kuelekea msimu mpya wa EPL wa mwaka 2021-2022.
Wawili hao watakutana kwenye mchezo wa heshima ya kufungua pazia rasmi la ligi hiyo ambayo inatimiza msimu wake wa 30 huku Brentford wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga Arsenal mabao 3-2 Juni 10 mwaka huu kwenye mchezo wa kirafiki.
EPL itaendelea tena siku ya Jumamosi ya kesho Agosti 14, 2021 kwa michezo saba ambapo makamu bingwa Manchester United itacheza na Leeds United saa 8:30 mchana, Chelsea watacheza nyumbani dhidi ya Crystal Palace, Southampton watasafiri kuwafuata Everton, Burnley watawakaribisha Brighton, Watford watakuwa wenyeji wa Aston Villa huku Wolves watakuwa wageni wa Leicester City huku michezo hiyo sita yote kupigwa saa 11:00 jioni.
Bingwa wa msimu juzi, klabu ya Liverpool itakuwa Anfield kuikaribisha Norwich City kwenye mchezo utakaochezwa saa 1:30 usiku kwenye muendelezo wa michezo itakayochezwa siku hiyo ya Jumamosi huku Newcastle United watakuwa na kibarua kigumu kuwavaa 'wagonga nyundo wa jiji la London', Westham United saa 10:30 jioni.
Bingwa mtetezi Manchester City atawafuta Tottenham Hotspurs kwenye mchezo unaotazamiwa kuwa wa kukata na shoka utakaochezwa saa 12:30 jioni mchezo ambao nyota mpya wa Manchester City, Jack Grealish ambaye pia anashikilia rekodi ya mchezaji ghali wa kiiengereza kutazamiwa kucheza mchezo wake wa kwanza.
Msimu huu wa 30 utakuwa ni msimu watatu kwa ligi hiyo pendwa Duniani kuendelea kutumia video ili kurejea matukio na kumsaidia mwamuzi afanye maamuzi sahihi yaani 'VAR' na utambulisho wa mapumziko mafupi ili kukabiriana na uchovu wa wachezaji.