Jumanne , 4th Aug , 2020

Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid ,Iker Casillas ametangaza kustaafu soka la ushindani akiwa na umri wa miaka 39.

Iker Casillas akiwa langoni pindi alipokua akiitumikia Real Madrid ya Hispania.

 

Casillas aliichezea Real Madrid michezo 725 akiwa na Real Madrid tangu akiwa na umri wa miaka 26,akishinda mataji matatu ya ligi ya mabingwa Ulaya na mataji matano ya La Liga.

Vile Vile aliisaidia Timu ya Taifa ya Hispania kushinda kombe la Dunia mwaka 2010 na pia kutwa mataji ya Ulaya mara mbili mfululizo kwa mwaka 2008 na 2012.

Aliutumikia Real Madrid kwa miaka 25 kabla ya mwaka 2005 kujiunga na Fc Porto ambayo kaichezea kwa miaka mitano.

Akiwa na Fc Porto alicheza michezo 156, na kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu pamoja na kombe la ligi mara moja.