Jumapili , 17th Jul , 2016

Ikiwa safari ya kushiriki mashindano makubwa ya baiskeli ya Tour of Rwanda imeiva, vyama vya mikoa vya mchezo huo, vimekumbushwa kuandaa mapema wachezaji wao kabla ya kuitwa timu ya Taifa.

Wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya mikoa, wametakiwa kuwanoa vijana wa mchezo wa baiskeli ili kurahisha kazi kwa kocha wa timu ya Taifa ya mchezo huo.

Mwenyekiti wa chama cha baiskeli Tanzania (CHABATA), Godfrey Mhagama, amesema vijana wakifundishwa mapema itakuwa kazi rahisi kufundisha vijana hao na si kupandisha viwango.

Tanzania inajiandaa na mashindano maarufu ya baiskeli ya Tour of Rwanda, yatakayofanyika mwezi Novemba mwaka huu, nchini Rwanda.