
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya kikosi cha Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
”Wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Coastal Union ambapo kila mchezaji yupo tayari kwaajili ya ushindi kwani msimu huu tumepanga kurudisha makombe yote.
“Clatous Chama, Ismail Sawadogo, Jean Baleke wapo tayari kwa mchezo na Peter Banda pia yupo tayari ikumbukwe kwamba walikosekana kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji,” Ahmed amesema.