Chelsea yanasa kiungo Mwafrika 

Alhamisi , 13th Feb , 2020

Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa kiungo Hakim Ziyech kutoka klabu ya Ajax ya nchini Uingereza.

Hakim Ziyech

Ajax imethibitisha kuwa kiungo huyo raia wa Morocco atajiunga baada ya kumalizika kwa msimu huu, mnamo Julai 1, 2020 baada ya Chelsea kufikia dau la Pauni milioni 45.

Katika ukurasa wa Twitter wa Ajax, umewekwa video inayoonesha maisha ya Ziyech ndani ya viunga vya klabu hiyo yenye mafanikio makubwa nchini Uholanzi, huku ikiambatana na ujumbe, "enyi Chelsea, muamini katika kipaji chake na vitu vikubwa zaidi vitakuja".