Jumatatu , 2nd Mar , 2015

Chama cha Mpira wa Wavu Dar es salaam DAREVA kimesema wameamua michuano ya Klabu Bingwa Mkoa wa Dar es salaam ichezwe kila mwishoni mwa wiki ili kuweza kutoa nafasi kwa vilabu mbalimbali shiriki vya ligi hiyo kuweza kupata nafasi ya kufanya mazoezi.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa DAREVA, Yusuph Mkarambati amesema michuano hiyo itakuwa ikifanyika kila jumamosi na jumapili ambapo mzunguko wa kwanza utamalizika Aprili mwaka huu huku mzunguko wa pili ambao ni wa kutafuta mshindi yatamalizika Agosti mwaka huu.

Mkarambati amesema, muda waliopewa wachezaji hao utawasaidia kuweza kufanya mazoezi na kuweza kuwa na ushindani mkubwa katika ligi hiyo ambapo wanaamini watapata wachezahi bora watakaoweza kuunda kikosi cha timu ya Taifa.